10 Aprili 2025 - 19:53
Source: Parstoday
Microsoft yalaaniwa kwa kumfuta kazi mhandisi aliyepinga mauaji ya kimbari Gaza

Shirika moja la kimataifa limelaani hatua ya kampuni ya Microsoft ya Marekani kumfuta kazi mhandisi wa programu mwenye asili ya Morocco, Ibtihal Aboussad, ambaye aliandamana hadharani kupinga uungwaji mkono wa kampuni hiyo kwa utawala katili wa Israel wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Microsoft.

Ijumaa wafanyakazi wa shirika la Microsoft la Marekani wameandamana wakati wa tukio la sherehe ya miaka 50 ya kuanzisha kampuni hiyo, wakitangaza upinzani wao dhidi ya kutumiwa teknolojia ya Akili Mnemba (Artificial Intelligence-AI-) ya kampuni hiyo na utawala wa Israel katika vita vyake vya mauaji ya kimbari huko Gaza.

Wakati wa hotuba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Microsoft AI, Mustafa Suleyman, Aboussad alipaza sauti na kusema:  na kusema: “Mustafa, aibu kwako,” huku akielekea jukwaani. Tukio hilo lilimfanya Suleyman aach hotuba yake.

Aliendelea kusema, “Wewe ni mfanyabiashara anayefaidika na vita. Acha kutumia Akili Mnemba kufanya mauaji.”

Bi. Aboussad akiwa amevalia Hijabu aliendelea kusema: “Unadai kwamba Akili Mnemba inatumiwa kwa ajili ya malengo mema, lakini Microsoft inaliuzia jeshi la Israel silaha za Akili Mnemba. Watu elfu hamsini wameuawa Gaza na Microsoft inashiriki katika mauaji hayo.”

Kupitia chapisho kwenye mtandao wa X (zamani Twitter), shirika la kimataifa Ansar al-Nabi limekosoa vikali Microsoft kwa kumfuta kazi Bi. Aboussad ambaye alikuwa akibainisha maoni yake.

Shirika hilo lilitoa wito kwa wafanyabiashara Waislamu na wamiliki wa makampuni makubwa pamoja na taasisi, kumfungulia Aboussad milango ya ajira na kumpa nafasi inayolingana na heshima yake.

"Msimamo wa kishujaa wa Aboussad uwe somo kwa vizazi, na kumkumbatia kwake kuwe heshima kwa ukweli. Ujumbe wetu uko wazi: Ummah wa Kiislamu haumwachi mtoto wake anayechagua njia ya heshima," taarifa hiyo ilieleza.

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, imepongeza misimamo ya baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Microsoft wakati wa sherehe ya miaka 50 ya kampuni hiyo ya teknolojia wakipinga ushiriki wa Microsoft katika vita vya mauaji ya halaiki vya jeshi la Israel katika Ukanda wa Gaza.

Taarifa ya Hamas imepongeza sana msimamo wa kishujaa wa mhandisi Aboussad, ambaye kwa ujasiri na kwa kujitolea, alifichua ushirikiano wa makampuni makubwa ya teknolojia ya kimataifa na mashine ya mauaji ya utawala wa Kizayuni kwa namna ya kipekee."

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha